Tuesday, December 18, 2012

MSANII MCHANGA AMWAMBIA SUMA MNAZALETI ''KAMA UMESHINDWA KAZI RUDISHA ELFU SABINI YANGU, PAMOJA BUKU NNE ZA BODABODA''

Mzee wa Kunonihino/ Suma Mnazaleti
Chukua Time Hit Maker, Suma Mnazaleti anadaiwa shilingi Elfu Sabini  na msanii Mchanga aliyejitambulisha kwa jina la Gee, inasemekana msanii huyo alimpatia Suma Mnazaleti Kiasi hicho cha Pesa ili ampigishe Collabo, lakini kinyume chake sasa ni miezi miwili imepita Suma hajaenda kuingiza sauti kwenye ngoma ya Dogo huyo ambaye anadai kuwa Pesa hiyo ameipata kwa Msoto, pia alimpa kaka yetu elfu nne za kupanda Bodaboda, na yeye alidhani maisha yatakua rahisi iwapo ngoma yake ingetoka huku akiwa amemshirikisha Star huyo, Dogo huyo amedai kuwa kila akimvutia wire Suma Mnazaleti anaambulia Sound Mvua, ndipo akaamua kumtafuta Mhariri Mkuu wa Gazeti La Makorokocho, Suma alipovutiwa Wire na Gossip Cop hakutoa Ushirikiano zaidi ya kuruka ruka viunzi na baadae akachima kwa kukata simu.
Skiza maongezi yalivyokua Kati yao:

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.